Monday, June 25, 2012

WASANII WACHOMA DAMU BILA CHAPAA-MISS LAKE ZONE INTER COLLEGE- KAGERA


Baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumsaka miss lake inter college kwa mkoa wa kagera yaliyofanyikajumamosi ya tarehe 23 Juni,2012, baadhi ya wasanii wa muziki waliotumbuiza katika shughuli hiyo iliyoonekana kufana, wametiririka na kusema hawakupewa chapaa.
Wasanii waliotumbuiza katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Khadija Kopa, wakati  wasanii wa nyumbani walikuwa ni Puya Man, Jimmy Yeyyo,na wengine wengi wanaochipukia.
Akiongea na FOR GOOD FOR MUSIC mitaa ya BK, mmoja wa wasanii hao alisema kuwa baada ya show, msimamizi wa kazi zima ambaye pia ilibidi awatoe wasanii hao mpunga, alitokomea mitini. Tetesi zinasema kuwa msimamizi huyo aliondoka kwa ndege ya asubuhi siku baada ya pamoja na mkongwe wa mipasho Khadija Kopa.
Kinachoonekana ni kwamba wasanii wa nyumbani ndio hawajapewa malipo ya namna yoyote.

Haijawekwa wazi kuhusiana makubaliano ya malipo kati ya mwandaaji na wasanii hao wa muziki, lakini uhakika kwamba hayakuwepo makubaliano ya kutumbuiza bure.
Harakati za kumpata msimamizi wa shughuli hiyo ambaye amejulikana kwa jina moja tu la JOSE zimegonga mwamba.
Swali kubwa ni kwamba, Hivi kweli mpaka zama hizi bado kuna watu wanaandaa show wakijarajia kuwaliza wasanii wa muziki? Iko wapi heshima ya msanii kama hadi leo hii msanii anapewa bia kabla ya show asubuhi yake hakuna wa kumpa supu na chake hajapata? Iko wapi mikataba ya kazi kwa wasanii?
Jamani waandaaji wa matamasha sio mpango huo, wasanii pia tuamke sio wakat wakuburuzwa tena.

No comments:

Post a Comment