Kampuni ya burudani ya LOOZE LINE ENTERTAINMENT, inayofanya kazi na wasanii kama Bonifasii, Stiba, WAKAWA, Saphire pamoja na wengine wengi natarajia kuachia nyimbo kadhaa za wasanii wake kuanzia mapema mwezi Julai 2012.
Wasanii watakao husika wanatarajia kuwa Stiba na Bonifasii ambao wamefanya vizuri na track yao ya UJIO KAMILI inayofanya vizuri katika mitandao mbalimbali ya muziki. Wakali wengine wanaotarajiwa kuachia ngoma ni pamoja na Saphire ambaye atakuwa introduced na LOOZE LINE baada ya kuachiwa mawe ya wakali wa crew ya WAKAWA. Taarifa toka studio zinasema track ya Stiba iko kwenye hatua za mwisho za mastering na track nyingine zinasubiria kumalizia vocals.

No comments:
Post a Comment