Kundi la Hip-hop MAPACHA wakiwemo mapacha K na D wa Maujanja Saplayaz, wakiongea kupitia Capital FM wameahidi kumsaidia Dogo Janja
aliyefukuzwa Tip Top Connection na kurudi Arusha wiki hii anapata haki
yake.
K amesema
sio haki msanii huyo mwenye umri mdogo kurudi nyumbani bila chochote
licha ya kuliingizia kundi hilo hela fedha za kutosha kutokana na show
alizokuwa akifanya.
“Haki ya Dogo Janja iko wapi? Kama anarudi Arusha bila ya chochote!
Madee imefika mahali lazima watu wajue ukweli maana maongezi yako kwenye
vyombo vya habari yanagongana. Kama kuna unyonyaji ulikuwa unaendelea
basi watanzania wajue na hatma ya huyo dogo ifikiwe na apewe haki yake.
Tumechoshwa na unyonyaji magenge ya mwenge,” aliandika K kupitia Facebook.
Dogo Janja yeye alisema ameamua kuondoka baada ya kuishi maisha ya tabu,
kudhulumiwa haki yake na kufanywa kama kitega uchumi cha kundi hil


No comments:
Post a Comment