Monday, May 21, 2012
T.I Kutema Game
Mkali wa Hip Hop T.I ameongea kwenye interview ya radio kuwa anataka kuacha muziki. T.I anasema mchezo umebadilika kutoka ulikoanzia na unapoelekea, na unakwenda kinyume na anachokiwakilisha yeye binafsi. Anaendelea kusema "katika muziki wa zamani tuliongea na watu wenye hisia kama zetu lakini sasa hivi tunaongea na watu wenye hisia tofauti na sisi. Zamani ku-rap juu ya vitu usivyovifanya lilikuwa jambo la ajabu lakini sasa hivi hakuna mtu anayetegemea uimbe juu ya uhalisia wa maisha yako, hili liko kinyume na mtazamo wangu, alisema T.I. Mkali huyo alimalizia kwa kusema' "Kama wataniondoa kwa mauzo , bora nisepe nirudi maisha yangu ya zamani ninyooshe miguu juu ya meza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment