DOGO JANJA ATUPIWA VIRAGO TIP TOP CONNECTION

Nyota
wa muziki wa kizazi kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye
maskani yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam Abdul Abubakar Chende
‘Dogo Janja’ ametupiwa
virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza na Teentz .com mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad
Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano
halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo
kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila siku badala
yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo
kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari
kwa safari ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba
yake kumuarifu kuwa Tip Top hatuko na mwanae kwa sasa” alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na
kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi kufuatia
mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection kwani hivi
karibuni alitega shule na kwenda kujificha nyumbani kwa TundaMan hukua
akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan
aliamaua kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa kundi aliamua
kwenda kumsaka, lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja
aliamua kukimbia na kwenda kujificha uchochoroni lakini akiwa huko
mafichoni bahati mabaya alikanyaga kuku na siri yake kujulikana kuwa
amejificha hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho chake
tayari kurejea ‘kileji’.
"vimekuwa ni vitendo vya kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'
No comments:
Post a Comment