Friday, July 27, 2012

JAYZ ASIFIWA NA SHOGA ELTON JOHN KWA KUUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA (aahidi kumkumbatia)

Msanii mkongwe wa muziki wa nchini Uingereza, ambaye pia ni shoga amemsifia sana Jayz, gwiji la hip hop baada ya gwiji huyo kuunga mkono ndoa za jinsia moja. Jayz alisema,"sio kwamba tu ni kosa kuzuia ndoa za jinsia moja, bali ubaguzi wa aina yoyote ile ni jambo baya"

Uungaji mkono wa Jayz kwa ndoa za jinsia moja umewashtua wengi, kwani ulimwengu haukutarajia mkongwe anayeheshimika sana katika hip hop, na ikizingatiwa kuwa ni mtu mweusi.

Kilichowashtusha sana watu ni kauli ya Elton John kumpa Jayz kumbatio kubwa pale tu akikutana nae. (When I see him I'm going to give him the biggest hug)

Suala la ndoa za jinsia mija limekuwa gumzo kubwa kwa siku za karibuni ikiwa ni pamoja na wasanii wakubwa kuliunga mkono suala hilo akiwemo 50 Cent.

No comments:

Post a Comment