Thursday, July 26, 2012

JOSE CHAMELION ATINGA UBALOZI WA UG-TZ KUDAI PASSPORT

Jose chammilione atinga ubalozi wa tanzania kwa maandamano kudai passport yake inayoshikiliwa na shigongo mwezi mzima!
Passport yake imechukuliwa baada ya muandaaji wa show 'Shigongo' kudai kuwa ametapeliwa katika show hiyo. Habari zinasema kuwa Shigongo alitapeliwa na waganda waliomualika Kampala na kutumia gari linalofanana na la Chamelion (Range Rover) nyeupe. Shigongo alitoa malipo ya awali kiasi cha dola za Kimarekani 3,500 kwa ajili ya show ya Dola 7,000.
Baada ya kuona kaingizwa mjini Shigongo alitumia gharama zake kumsafirisha Jose kama mbinu ya kumbana akishafika Dar, na ndo akafanikiwa kuizuia passport.
Inasemekana mawasiliano ya show hiyo yalifanyika kupitia kwa msanii mkali wa Burundi Kidumu ambaye kwa mara ya kwanza ndiye aliyemwambia Jose juu ya habari ya kufanya show Dar TZ

Kwa taarifa ni kwamba Chamelion kaondoka TZ kwa kibali cha muda mfupi, na baada ya kufika Uganda kaenda kupeleka malalamiko yake katika ubalozi wa Tanzania nchini Uganda

No comments:

Post a Comment