Monday, May 21, 2012

YOUNG BUCK ATIMULIWA NYUMBANI KWAKE

Msanii wa Hip Hop Young Buck ambaye pia ni moja kati ya wasanii walioipaisha G-UNIT hadi kukonga nyoyo za mashabiki wa Hip Hop duniani kote, juzi ameonekana akifungasha vifurushi na kuyaacha makazi yake kwa kile kinachosemekana kuwa anadaiwa kiasi cha dola za kimarekani 333,975.69 za kodi. 

Buck alitakiwa kumaliza pango lake tarehe 15 Mei, 2012. Mpaka sasa yeye mhusika hajaweka wazi kama kweli kaondoka kwa kudaiwa au la. Mahakama tayari imeishathamanisha nyumba tayari kwa kuiuza ili kufidia deni la kodi. Hata hivyo taarifa ya mahakama haijaongelea sababu za kumwondoa mkali huyo ndani ya nyumba hiyo.

Habari nyingine pia mwisho wa wiki iliyopita zinasema kuwa msanii huyo wa zamani wa G-UNIT atafungwa jela kwa kipindi cha miezi miwili japo sababu hazijajulikana bado pia, Buck kathibitisha kuwa ataenda jela.

1 comment:

  1. xo style kama jamaa kafulia hivi daah habari yake bhana

    ReplyDelete